Na Veronica Kazimoto, Dar es Salaam
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) imekanusha habari inayosambaa katika mitandao ya kijamii ikidai kuwa TRA kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha na Mipango pamoja na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), inatangaza nafasi za kazi 500 za uelimishaji wa namna ya uchangiaji kodi pamoja na ukusanyaji wa Kodi ya Majengo vijijini.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Huduma na Elimu kwa Mlipakodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, wananchi wameombwa kuipuuza habari hiyo.
“TRA inakanusha taarifa hiyo na inauomba umma kuipuuza kwa sababu haina ukweli wowote”. Ilifafanua taarifa hiyo.
Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, hata mawasiliano yaliyopo kwenye habari hiyo potofu siyo mawasiliano rasmi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania hivyo wananchi wanatakiwa kuwa makini ili kuepuka kutapeliwa.
Kumekuwepo na taarifa inayosambaa katika mitandao ya kijamii yenye kichwa cha habari “Mamlaka ya Mapato Tanzania (Tanzania Revenue Authority) kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha pamoja na Benki Kuu (BOT)”, ikieleza kuhusu TRA kutangaza ajira 500 ambayo imesababisha mamlaka hiyo kukanusha na kuwatahadharisha wananchi kuhusu taarifa hiyo potofu.
TRA imewaomba wananchi kupiga simu bure Kituo cha Huduma kwa Wateja kupitia namba 0800 750 075 au 0800 780 078 au kutuma barua pepe: huduma@tra.go.tz, au kutembelea tovuti ya Mamlaka ya Mapato Tanzania: www.tra.go.tz. Pia, wanaweza kutuma ujumbe kwa njia ya WhatsApp kwenda namba 0744-233-333 ili kupata ufafanuzi wa masuala yoyote yanayoihusu mamlaka hiyo.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2KRiQqw
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







