* Wanafunzi, walimu na wadau mbalimbali wanaoshiriki kuiinua sekta ya elimu kupata tuzo hizo
KWA mara ya kwanza Kampuni ya Elimu Solutions Tanzania imeandaa tuzo za Tanzania Elimu Awards zitakazotolewa Agosti 31 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam huku mgeni rasmi akitegemewa kuwa Waziri wa nchi ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Seleiman Jaffo (Mbunge.)
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mkurugenzi Mtendaji wa Elimu Solution nchini Neithan Swedi amesema kuwa jukumu la kusaidia sekta ya elimu ni la kwetu zote, na serikali imeonesha mfano kwa kushiriki vyema katika sekta ya elimu na mwaka huu shule za serikali zimeingia katika shule kumi bora zilizofanya vizuri zaidi katika mitihani ya kidato cha sita.
Amesema kuwa wameanzisha utoaji tuzo za Tanzania Elimu Awards kwa walimu, wanafunzi na wadau wa sekta hiyo Afrika Mashariki na hiyo ni katika kuendeleza na kusimamia sekta hiyo muhimu katika ujenzi wa taifa na kueleza kuwa ni muhimu kuendeleza sekta hiyo ili iendelee kuwa kiwanda cha kuzalisha vijana wa kitanzania ambao ndio taifa la kesho.
Kwa upande wake msimamizi wa miradi kutoka Elimu Solutions Tanzania Peter Godian amesema kuwa katika kuenzi na kuheshimu jitihada za wanafunzi, walimu, shule, serikali na taasisi mbalimbali kampuni hiyo kwa mara kwanza imeandaa tuzo hizo ili kuleta motisha ili kuipeleka sekta hiyo mbele zaidi.
Amesema kuwa tuzo hizo TEA zinajumuisha tuzo 32 kutoka vipengele vikuu 11 zikiwemo tuzo kwa wanafunzi Bora wakike na kiume kwa shule za msingi na sekondari pamoja na vipengele mbalimbali vikiwemo walimu bora, shule bora, na tuzo ya heshima.
Amesema kuwa washindi watapatikana kupitia takwimu zitakazopatikama kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya elimu na wanaamini itachangia katika kuchangia utamaduni wa kutunza na kutambua mchango wa wasomi, wabunifu na wadau wa sekta ya elimu na kuzidi kuwapa faraja na moyo wa kuendelea kufanya kazi na kukuza sekta adhimu ya elimu.

Mkurugenzi Mtendaji wa Elimu Solutions Tanzania Neithan Swedi akizungumzia kuhusu utoaji wa Tuzo zijulikanazo kama Tanzania Elimu Awards zitakazotolewa na Kampuni hiyo zitakazofanyika Agosti 31, 2019 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msimamizi wa Miradi kutoka Elimu Solutions Tanzania Peter Godian na Kulia ni Afisa Masoko wa Elimu Solutions Tanzania Catherine Ndosi.
Msimamizi wa Miradi kutoka Elimu Solutions Tanzania Peter Godian akisoma tuzo zitakazotolewa na kampuni ya Elimu Solutions Tanzania kwenye hafla ya utoaji wa Tuzo zijulikanazo kama Tanzania Elimu Awards zitakazofanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam. Kulia ni Afisa Masoko wa Elimu Solutions Tanzania Catherine Ndosi na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Elimu Solutions Tanzania Neithan Swedi.
Afisa Masoko wa Elimu Solutions Tanzania Catherine Ndosi akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kapuni hiyo ilivyojipanga kutekeleza utoaji wa tuzo hizo wakati wa kutangaza utoaji wa tuzi zijulikanazo kama Tanzania Elimu Awards
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/345bVTi
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33