JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAJI
Dodoma: 03 Oktoba, 2019
Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Morogoro (MORUWASA)imevunjwa. Hatua hiyo imechukuliwa na Waziri wa Maji Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) kuanzia tarehe 02 Oktoba, 2019.
Taarifa ya Katibu Mkuu, Wizara ya Maji Prof. Kitila Mkumbo imeainisha kuwa kuvunjwa kwa bodi hiyo ni kwa mamlaka aliyo nayo Waziri wa Maji kwa mujibu wa kifungu Namba 14 cha Jedwali la kwanza la Sheria ya Huduma za Maji na Usafi wa Mazingira Namba 5 ya Mwaka 2019, kikisomwa pamoja na Kanuni Na. 14 ya Kanuni za Usambazaji wa Maji (Tangazo la Serikali Na. 90 la tarehe 26/04/2019).
Taarifa hiyo imefafanua kuwa bodi ya MORUWASA imevunjwa kwa kushindwa kutekeleza majukumu yake ya kuisimamia mamlaka ya maji hivyo kuathiri utoaji wa huduma za majisafi na usafi wa mazingira katika manispaa ya Morogoro.
Aidha, wakati huo huo Waziri wa Maji Mhe. Prof. Makame Mbarawa (Mb) ametaka kuanza kwa utaratibu utakaowezesha kuundwa kwa bodi mpya.
Kitengo cha Mawasiliano
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2n8MYpD
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33





