Na Woinde shizza Michuzi Tv , Arusha
Mgogoro wa Muda mrefu uliokuwa ukifukuta baina ya familia za Marehemu bilionea Erasto Msuya wa kugombea Mali umechukua sura mpya mara baada ya serikali ya Mkoa kuingilia kati kwa lengo la kupata suluhu ya kudumu nje ya Mahakama.
Mgogoro huo ambao umedumu kwa takribani miaka 7 tangia kifo cha Marehemu mwaka 2013, upande wa wazazi wa marehemu Erasto msuya na upande wa Mke wa marehemu Erasto aitwaye Miriam Erasto ambaye kwa sasa yupo mahabusu Gerezani kwa tuhuma ya mauaji ya WiFi yake,wameshindwa kuelewana juu ya rasilimali zilizoachwa na marehemu.
Akiongea na familia hizo katika nyumba aliyokuwa akiishi Marehemu Erasto iliyopo Kwa Iddy wilayani Arumeru,Mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro amewataka watoto wa marehemu waliokuwa wameikimbia nyumba ya marehemu baba yao wakihofia kuuawa kurejea katika nyumba hiyo kuanzia Leo wakati wakiendelea na utatuzi wa mtafaruku uliopo.
Aidha Muro amezitaka pande hizo mbili kufika ofisini kwake siku ya jumatatu SAA 4 asubuhi wakiwa wameambatana na vielelezo mbalimbali ili kufikia mwafaka wa mgogoro huo nje ya Mahakama.
“Si nia ya serikali kuingilia jambo lililopo mahakamani ila kama serikali tunamamlaka ya kusuluhisha jambo iwapo pande zote zipi tayari kuketi kwani suala la kutafuta msindi mahakamani si suluhu ya kuleta amani” Amesema Muro
Akiongea mgogoro huo mtoto mkubwa wa marehemu , aitwaye Kervin Erasto alimweleza mkuu huyo wa Wilaya kuwa wazazi wa marehemu baba yake( bibi) aitwaye Ndeshu Msuya na babu yake aitwaye Elisaria Elia Msuya pamoja na shangazi zake wanataka kumpokonya Mali za Marehemu baba yake .
Akijibu tuhuma hizo,Mama wa marehemu Erasto,Ndeshu Msuya amesema kuwa wao kama wazazi wa marehemu Erasto hawana nia ya kutaka urithi wa mali yoyote ya marehemu mtoto wao ila wanasikia uchungu kuona Mke wa Erasto akiuza Mali ovyo za Marehemu mtoto wao ili kumaliza suala la kesi ya mauaji inayomhusu wakati ugawanyo wa Mali bado haujafikiwa.
Mama huyo amedai kuhofika watoto wa marehemu kupoteza rasilimali hizo kutokana na Mali hizo ndugu wa Mke kujimilikisha ambao wamejipa kipaumbele kusimamia jambo ambalo linawapa mashaka kwamba huenda watoto hao wakadhulumiwa.
Naye baba wa marehemu aitwaye Elisaria Msuya amesema madai yanayotolewa kuwa amejimilikisha mgodi wa marehemu Erasto hayana msingi wowote kwani wakati anamzaa Erasto alikuwa anamiliki migodi huko Mererani na ubilionea wa Msuya umetokana na yeye kumpa mgodi wa kuchimba madini ya Tanzanite.
Marehemu Erasto alifariki agosti,7mwaka 2013 kwa kupigwa risasi zaidi ya 20 eneo la Mijohoroni,wilaya ya Hai ,mkoani Kilimanjaro na watu ambao baadae walikamatwa na kuhukumiwa kifungo cha maisha jela Mara baada ya Mahakama kuwatia hatiani.
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Jerry Muro (pili kushoto) akiwa na familia ya marehemu bilionea Erasto Msuya
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/33Ary4a
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







