Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amewaapisha Viongozi mbalimbali Ikulu jijini Dar es Salaam leo, ambao ni Mdhibiti na Mkaguzi mkuu wa Hesabu za serikali, Katibu Tawala, Balozi, Kamishna wa kazi katika ofisi ya Waziri Mkuu, na Majaji 12 wa mahakama kuu pamoja na Mwenyekiti, na makamu mwenyekiti na Makamishna watano wa Tume ya Haki za binadamu na utawala bora.
Akizungumza na viongozi hao wateule, Rais Magufuli amesema kuwa walioteuliwa wasidhani kuwa hizo ndio nafasi zao moja kwa moja, Pia amewashauri majaji wakafanye kazi kwa haki bila kumuonea Mtu, kwani hukumu hutolewa na Mungu tu, ila kwa hapa duniani tunao Majaji.
“Kuna watu ukiwateua wanadhani hizo ndio nafasi zao moja kwa moja, wewe (CAG) nilipokutoa toka kuwa Mkurugenzi wa TRA (Mamlaka ya Mapato Tanzania) kwenda kuwa Katibu Tawala mkoa hukusema neno na ulikuwa mtulivu ,wapo wengine ukiwatoa wanasema maneno maneno, wakati huo unapowateua huwa hawasemi” Amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli amemuasa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kutokuwaonea watu pale anapopewa maagizo na mihimili mingine kama Bunge na Mahakama, akatekeleze majukumu yake kwani yeye ni mtumishi na asibishane.
“Najua CAG una ‘Qualification’ nzuri tu na huwa hatufanyi makosa tunapoteua, form four ulitoka na divison one, form six ukatoka na division one hii ni kuonesha wewe ni kipanga sio kilaza, ‘Degree’ ya sheria unayo, ukachukua na masters, umefanya kazi sehemu nyingi tu” Amesema Rais Magufuli.
Rais Dkt John Pombe Magufuli leo Novemba 4,2019 amemuapisha Charles Kichere kuwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kufuatia uteuzi alioufanya hapo jana. Hafla ya kumuapisha Kichere ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Katibu Tawala wa mkoa wa Njombe pamoja na viongozi wengine, imefanyika Ikulu Jijini Dar es salaam.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2WFqmtZ
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







