MKUU wa Mkoa wa Manyara, Alexander Mnyeti amewakabidhi pikipiki watendaji sita kati ya nane wa Kata za Mjini Babati, waliokuwa wanafanya kazi zao kwa changamoto ya ukosefu wa usafiri, ili kuwafikia na kuwatumikia wananchi wengi zaidi.
Pikipiki hizo sita zenye thamani ya sh14.3 milioni zimenunuliwa na halmashauri ya mji wa Babati, kupitia fedha za kujenga uwezo zinazotokana na kuendeleza miji (ULGSP).
Mnyeti akiwakabidhi maofisa watendaji hao wa kata sita za mjini Babati, alisema vitendea kazi hivyo viwe nyenzo za kuwafikia wananchi zaidi tofauti na awali.
Alisema watendaji kata hao waliopo pembezoni mwa mji wa Babati wanapaswa kutokaa ofisini na kuwafikia wananchi kuwatumikia ili kuondokana na kisingizio cha ukosefu wa usafiri.
“Tunataka tuone kero za wananchi zinatatuliwa, kama mimi nafika hadi vijijini, ninyi watendaji wa kata au vijiji mnapaswa kufika hadi kwenye ngazi ya kaya na kutatua changamoto zao,” alisema Mnyeti.
Hata hivyo, alimuagiza mkurugenzi wa mji wa Babati, Fortunatus Fwema kuhakikisha maofisa watendaji wa kata za Babati na Bagara, nao wananunuliwa pikipiki kama wenzao.
Fwema alisema wapo kwenye mchakato wa kuhakikisha wanawanunulia pikipiki watendaji wa kata za Babati na Bagara. “Baada ya kuwanunulia pikipiki watendaji wa kata zilizo pembezoni tunaahidi kutekeleza agizo lako la kuwanunulia watendaji wawili wa Babati na Bagara ili kukamilisha kata zote nane,” alisema Fwema.
Ofisa utumishi wa halmashauri ya mji wa Babati, Sadiki Mrisho alisema pikipiki hizo zinapaswa kutumiwa na maofisa watendaji wa kata sita kwa matumizi ya serikali pekee. Mrisho alisema pikipiki hizo zimetolewa kwa mkopo kwa watendaji hao utakaosaidia utunzaji na ununuzi wa pikipiki nyingine.
Ofisa mtendaji wa kata ya Sigino, Evelin Panga alisema pikipiki hizo zitawasaidia kufika kiurahisi katika shughuli zao vijijini.
Panga aliishukuru serikali kwa kuwapatia nyenzo hizo za usafiri kwani awali walikuwa wanatembea kwa miguu kutoka sehemu moja hadi nyingine.
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/32u6StJ
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







