Na Woinde Shizza,Globu ya Jamii Arusha
MKUU wa Wilaya ya Longido Frank Mwaisumbe ameongoza operesheni ya kuwakamata waahamiaji haramu kotoka nchini Somalia wakiwa na ngamia 200 pamoja nyaraka mbalimbali kutoka nchi ya Kenya.
Akizungumza leo wilayani hapa mara baada ya kuwakamata baadhi ya wahamiaji hao haramu
kutoka nchini Somalia,Mkuu huyo wa Wilaya wamefanikiwa kuwakamata baada ya kupata taarifa kuwa katika mpaka wetu wa Namanga upande wa Magharibi ndani ya kata ya Kimkoa ambayo ina karibu kilometa 30 kutoka Mjini Namanga kuna watu wasiojulikana wameweka makazi(kempu).
Amesema baada ya kupata taarifa hizo walikwenda kufanya operesheni na kufanikiwa kuwakamata watu wawili wenye asili ya nchi ya Somalia na hakuwa na uwezo wa kuzungumza lugha ya Kiswahili huku wengine wao wakiwa wamekimbia
“Tulienda na Kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya pamoja na baadhi ya askari kutoka mkoani, katika eneo hilo tumefanikiwa kuwakamata wahamiaji hao haramu wawili.Wengine wamekimbia,”amesema Mkuu wa Wilaya Mwaisumbe
Amefafanua baada ya kuwakamata walifanikiwa kuwakuta na mifugo aina ya na ngamia zaidi ya 200 pamoja na nyaraka mbalimbali kutoka nchi ya jirani ya Kenya.
Amesema kuwa operesheni hiyo haitaishia hapo bali itaendelea kwa lengo la kuhakikisha watu wote ambao wameingia nchini bila utararibu na kuweka makazi ya kudumu wanachukuliwa hatua na kutoa rai kwa wananchi kutoa taarifa wanapoona kuna watu wameingia nchini kwetu.
Wakati huo huo Mwaisumbe amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo na kamati ya ulinzi na usalama wa mkoa kwa ushirikiano ambao umefanikisha kukamatwa kwa watu hao pamoja na mifugo yao ya ngamia.Kwa upande wake Mkaguzi wa Uhamiaji ambaye ni Mkuu wa Kitengo cha
Udhibiti na Usimamizi wa mipaka Mkosa wa Arusha Elisamia Mmari amesema kwa utaratibu wa uhamiaji watuhumiwa hawa watapelekwa katika ofisi za uhamiaji na watachukuliwa maelezo baada ya hapo watafikishwa katika vyombo vya sheria ili iwefundisho kwa watu wote wanaiongia nchini na kufanya shuhuli za bila kufata taratibu.
Mwisho
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/2Ct9DAV
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







