Na.Khadija seif, Michuzi TV
MSANII wa Bongofleva Nasib Abdul a.k.a Diamond platinum amewapongeza wasanii,makampuni pamoja na vyombo vya habari kwa kufanikisha tamasha la wasafi lililofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita.
Diamond amesema hayo katika ukumbi wa Hyatt regency uliopo jijini Dar es salaam ,nakugusia swala la wasanii hao kutoka nchi ya Nigeria kuwepo kwao kulikua na lengo maalumu.
“Lengo lilikua ni kujifunza kwa wenzetu jinsi ya kutumbuiza kwao kwa kuona mubashara tofauti na wengi wetu tulikua tunaona tu kupitia televisheni au kwenye mitandao ya kijamii,”
Aidha,mbali na kujifunza kutoka kwa wasanii hao wawili Diamond amefafanua zaidi kuwa wizkid na tiwasavage wataweza kututangaza kuanzia siku walipofika,sehemu watakazotembelea ,hivyo kutaleta ushawishi kwa watu ambao wanawatazama kutamani kufika nchi ya Tanzania.
Hata hivyo amewaomba wadhamini mwakani msimu mwingine wa Tamash hilo kuwaongezea fedha ili waweze kuwa na nafasi ya wasanii wengine kushiriki kikamilifu.
“Japo fedha ilikua pungufu sio sana lakini niliweza kutazama baadhi ya wasanii kwa jicho la kipekee kutokana na mara nyingi kutopewa nafasi kwenye majukwaa mbalimbali na ndio sababu pia sisi Kama wasafi na uongozi wa lebo yetu Wcb kuwapa nafasi wakongwe wa Muziki akiwemo inspector harun,Mandojo na domokaya,Madee na wengine kutumbuiza jukwaa la wasafi,”
Pia ametoa ushauri kwa wasanii kutosikiliza minong’ong’ono ya mashabiki zao wenye lengo la kuwagombanisha hasa mitandaoni.
“Wakati mwengine Mashabiki zetu wanatufanya tugombane ,tuchukiane na hata kutoelewana tuyapuuzie hayo kwani wote wanapenda kazi zetu kiujumla akitokea kwenye tamasha langu ataimba nyimbo zangu na akija kwako ataimba na zako huoni Kama wote Ni shabiki zetu tusiweke matabaka,”
from MICHUZI BLOG https://ift.tt/34Tn8WY
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







