Gauni hilo la Calvin Klein lililotengenezwa maalum kwaajili ya Lupita,
lilimvutia mwizi huyo kulinyemelea na kuliiba baada ya kudaiwa kuwa na
thamani ya $150,000 (zaidi ya shilingi milioni 274).
Mwizi huyo aliwapigia simu mtandao wa TMZ na kuwaelekeza alipoliacha
begi lenye gauni hilo, na TMZ walitoa taarifa polisi ambao walilifatilia
na kulikuta limerudishwa hotelini lilipoibiwa lakini likiwa limewekwa
bafuni chini ya sinki.
Mtu huyo aliiambia TMZ kuwa aliliiba gauni hilo kwenye chumba cha Lupita
baada ya kukuta mlango ukiwa wazi, na kubandua vigolori viwili na
kuvipeleka kwa wataalam wambao walimwambia ni za bandia.
Mwizi huyo aliongeza kuwa aliamua kurudisha gauni hilo na kuwapigia simu
TMZ ili kuumbua uongo wa mastaa wa Hollywood, na ulimwengu ujue kuwa
gauni hilo halina thamani iliyotajwa.