katika Mapenzi kuna vitu vingi unaweza
kumfanyia Mpenzi wako ukamfurahisha na kumfanya azidishe Mapenzi ila
katika safu hii nitazungumzia Mambo machache muhimu yatakayokusaidia
kuboresha na kudumisha penzi lako kwa umpendae
KARIBU:
YAFUATAYO NI MAMBO MUHIMU YANAYOZIDISHA UPENDO:
1.KUMNUNULIA ZAWADI MPENZI WAKO:
»
Zawadi ni moja ya sehemu husika katika
Mapenzi inayoweza kufanya penzi likawa bora na lenye kupendeza siku
zote, faham kwamba hakuna mtu asiependa kupewa zawadi na kila anaepewa
zawadi siku zote hujihisi kama ni mtu anaependwa na anaejaliwa na
kuthaminiwa hususani katika ulimwengu wa Mapenzi unapompa mpenzi wako
zawadi basi faham ya kwamba utamfanya mpenzi wako ajione kama ni wapekee
kwako na anathamani kubwa kwako hivyo hatosita kudhihirisha mapenzi
yake kwako, kikubwa zingatia pindi unaponunua zawadi kwa ajili ya kumpa
mpenzi wako jitahidi kuwa mbunifu na uwe ni mwenye kubadilika sio kila
siku zawadi zile zile zinajirudia kwa kufanya hivi utamboa mpenzi wako
kuwa mbunifu na jaribu kumpa mpenzi wako zawadi zenye kutunzika mfano
kama Card, maua, nguo n.k. Utamfanya azidi kukupenda zaidi na zaidi.
2. MSIFIE MPENZI WAKO:
»
Sifa zinaleta changamoto katika mapenzi.
Unapaswa kutambua kuwa usiwe mchoyo wa sifa kwa mpenzi wako usisubiri
watu wapembeni wamsifie mpenzi wako pindi anapofanya jambo zuri na lenye
kupendeza chukua nafasi hii wewe kama kioo chake unadhani usipo msifia
mwenza wako unataka nani amsifie?! Jitahidi kudhihirisha sifa kwa mpenzi
wako kwa mfano umemuona mpenzi wako kapendeza basi usisite kumwambia
“Sweetie nimependa vazi lako la leo ama hakika umetoka sex nakutamani
zaidi ya siku zote navyokutamani ingawa siku zote unaziteka hisia zangu
ila leo ni zaidi” unaweza kumpa maneno kama haya na mengine mazuri ya
kuvutia, sifa zipo nyingi mbali na kumsifu mavazi yake hata tabia n.k.
Kwa kufanya hivi utamfanya mpenzi wako azidishe mapenzi kwako kwani
atahisi kampata mtu anaejali ubora na uhalisia wake kimaumbile na
kimatendo. ZINGATIA:- Usitoe sifa ilimradi sifa zisizo na ukweli.
3. EPUKA KUMUUDHI MPENZI WAKO:
»
Sote tunafahamu kuwa hakuna binadamu
aliekamilika na hakuna alietolewa nyongo kila mtu anakasirika na
anakosea ila solution kubwa ni kudhibiti hasira na kurekebisha makosa na
kusuluhisha hususani kwenye mapenzi, katika mapenzi hakuna jambo baya
linalopunguza upendo kama ugomvi na kumuudhi mpenzi wako mara kwa mara.
Ili kuboresha mapenzi na kulifanya penzi lako liwe imara na lenye
kuvutia basi jitahidi kuepuka kumuudhi mpenzi wako na pindi ikitokea
umekorofishana na mpenzi wako jaribu kutafuta suluhu mwite kaa nae
muombe samahani iwapo kama unakosa na hata ikitokea kosa si lako pengine
kakuudhi na bado unamuhitaji usikae na kinyongo wala usiumize nafsi
yako kaeni muyamalize muendeleze mahusiano yenu na msiwe watu wa
kuzungumzia tofauti zenu kwa watu wa pembeni. Kwa kufanya hivi daima
mtakuwa ni mfano mzuri wa kuigwa na mapenzi yenu hayatofika kikomo zaidi
yataendelea kushamiri.
4. MFANYIE YATAKAYO MFURAHISHA:
»
Kuna mambo mengi mazuri na yakuvutia
katika mapenzi unaweza kuyafanya kwa mpenzi wako yakamfurahisha kwa
mfano unaweza kusoma tabia ya mpenzi wako na ukajua ni nini anapenda na
kipi hapendi kufanyiwa ukajitahidi kujilinda kumtendea asiyoyapenda na
ukaufungua moyo wako kwa kumridhisha kumfanyia kile anachokipenda.
Katika mapenzi watu wengi hupenda kutolewa Out, kupewa ofa ya lanch,
kupewa zawadi zenye mvuto na zenye hamasa nzuri kwenye mapenzi. Unaweza
kufanya vitu vizuri vyenye kuvutia kwa mpenzi wako vikamvutia ikawa ni
nafasi nzuri kwako kumfanya azidishe mapenzi.
5. KUWA MTU WA UTANI KWAKE:
»
mpenzi msomaji ninapozingumzia mapenzi na
maanisha mazoea yaliyoambatana na upendo, siku zote mapenzi hujijenga
moyoni kwa mtu kutokana na ukaribu na mazoea yaliyopo baina ya watu
wawili, katika pointi hii ya mwisho nataka nizungumzie utani katika
mapenzi unafaida gani. Mpenzi msomaji fahamu yakuwa utani ni moja ya
sehemu katika mapenzi na utani unasaidia kuboresha mapenzi ila utani
ninaotaka kuuzungumzia hapa ni utani wa kawaida na sio ule wa kuvuka
mipaka. Elewa wazi kabisa unapokuwa na mpenzi wako na ukawa ni mtu wa
utani inakusaidia wewe kumfanya mpenzi wako akuzoee na awe anajisikia
kuwa karibu nawewe muda wote kwani utakuwa unamfurahisha kutokana na
utani wako. ZINGATIA:- Usivuke mipaka ya utani, usimtanie kupitiliza,
mtanie kutokana na mazingira, usiwe utani unaofanana nakweli, mtanie kwa
faida.
MPENZI MSOMAJI WA KURASA HII UKIZINGATIA
HAYA MACHACHE YALIYOANDIKWA NA UKATEKELEZA KAMA ILIVYO AGIZWA SIDHANI
KAMA PENZI LAKO KWA UMPENDAE LITATETEREKA NA KUTAWALIWA NA SUMU YA
PENZI. Siku zote Penzi litabaki kuwa imara na lenye kuvutia kwako na kwa
watu wa pembeni. Mapenzi sio mitishamba dawa ya Mapenzi unayo wewe
mwenyewe.