
Julai 13, 2020 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa katika uwanja wa ndege wa Nachingwea alipokea mchango huo kwa niaba ya Rais Dkt. Magufuli kutoka kwa wazee hao.
Akitoa salamu hizo kwa niaba ya Rais Dkt. Magufuli, leo mchana (Jumanne, Julai 21, 2020), katika uwanja wa ndege wa Nachingwea Mkoani Lindi, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema Rais Magufuli amefarijika sana kwa mchango huo.
“Rais amesema aliniona wakati napokea salamu kutoka kwa wazee hapa uwanja wa ndege Nachingwea, mkanikabidhi mchango kwa ajili yake, anawashukuru sana na salamu zenu amezipokea kwa mikono miwili,” amesema.
Amesema Rais Magufuli anawashukuru kwa kupata wazo hilo na amewataka waendelee na majukumu yao na ameahidi kuzunguka maeneo yote nchini ili kuwapa mrejesho wa utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya mwaka 2015 – 2020.
Akizungumzia mchakato wa kura za maoni ndani ya CCM, Mheshimiwa Majaliwa , amewapongeza wana CCM waliojitokeza kwa wingi kuomba ridhaa ya kuteuliwa kuipeperusha bendera ya CCM katika Uchaguzi Mkuu ujao na amewataka waendelea kuwa wamoja.
“Endeleeni kuwa wamoja hata baada ya mchakato wa kumpata mgombea mmoja wa kupeperusha bendera ya CCM kukamilika na ninawasihihi wote muungeni mkono mgombea huyo ili kujenga mshikamano na kukipa Chama ushindi,” amesema.
Mheshimiwa Majaliwa alisema hayo baada ya kubaini kuwa miongoni mwa wananchi waliojitokeza kwenye Uwanja wa Ndegewa nachingwea kumuaga wakati akitoka Ruangwa kurejea Dodoma ni Wan CCM waliojitokeza kuomba ridhaa ya Chama kwa nafasi ya ubunge na ambao wamemaliza mchakato wa awali wa kupigiwa kura.
*Wakati huohuo* , Waziri Mkuu amewataka viongozi wa Chama na Serikali wahakikishe wanawahamasisha wananchi kufanya kazi za kujiletea maendeleo ikiwemo kujihusisha kwenye kilimo na biashara.
“Ndugu zangu tuendelee kuhamasisha Watanzania na wana- Nachingwea wafanye kazi kwa bidii, lazima kila kaya ijiridhishe inakuwa na chakula cha kutosha lakini pia ilime mazao ya kibiashara kama korosho, ufuta, alizeti na mazao mengine, kila mmoja awe na akiba ya kutosha ya mazao ya chakula na biashara.”
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






