Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo amesema CCM haiko tayari kuacha kuhoji na kufuatilia kwa Ukaribu Miradi mbalimbali ya Kimaendeleo na Kimkakati inayotekelezwa na Serikali.
Chongolo ametoa Kauli hiyo leo Januari 30, 2023 katika Kata ya Dumila, Wilaya ya Kilosa aliposhiriki kikao cha Shina namba 10, ikiwa ni Siku ya tatu ya Ziara yake mkoani Morogoro, ambapo pia alipata nafasi ya kusikiliza kero na Changamoto mbalimbali za Wananchi kwenye Kata hiyo.
Amesema CCM ndio Chama kinachoongoza Serikali ya Sasa iliyopo Madarakani, Serikali inayoongozwa na Mwenyekiti wa CCM na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, hivyo ni Jukumu lake kuendelea kuhoji na kufuatilia kwa Sababu ndio kimepewa dhamana ya Kuwaongoza Watanzania.
“Kuna Jamaa Wajanja wanataka tusihoji wala kufuatilia, Sisi lazima tufuatilie, tuhoji na tuambiane ukweli hadi kieleweke kwa Sababu CCM ndio iliyopewa Dhamana na Wananchi ya kuongoza nchi” amesema Katibu Mkuu Daniel Chongolo.
Aidha Chongolo amesema Chama cha Mapinduzi (CCM), hakiko tayari kuharibikiwa ndio maana kinapita kwa Wananchi na kila eneo ili kutimiza wajibu wake kwa Watanzania ili kuona kama Ilani yake ya Uchaguzi ya Mwaka 2020-2025 inatekelezwa kikamilifu.
Katibu Mkuu Chongolo akifafanua zaidi Ameeleza kuwa CCM ni kama Mmiliki wa Duka, kwani mwaka 2019/2020 ndio kilipita kwa wananchi na kuomba dhamana ya kuunda serikali, hivyo serikali ni kama wauza duka na wenye duka ni CCM hivyo ni lazima tupite kukagua na kutazama maendeleo na utekelezaji wa ahadi zote tulizo ahidi kwa kujionea namna wananchi wanavyopewa huduma na serikali.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33









