MWANAMKE Ukiwa na Tabia Hizi 7, Lazima Mwanaume Akukimbie

Admin Updates2 years ago6 Views

 MWANAMKE Ukiwa na Tabia Hizi 7, Lazima Mwanaume Akukimbie

1. CHOKOCHOKO
Wanaume wengi huwa hawapendi chokochoko. Hawapendi mwanamke ambaye yeye kila wakati ni kuanzisha chokochoko ambazo zinazalisha ugomvi. Wanaume wengi hawapendi mabishano. Hawapendi ugomvi hivyo mwanamke anapokuwa hodari wa kuleta chokochoko, huepukwa.

Ni vyema basi mwanamke akachunga kauli. Akawa si mtu wa kuchimbachimba vitu ambavyo havina kichwa wala miguu. Asiwe na kisirani. Kinywa chake kitawaliwe na maneno matamu, yatakayomtia moyo mpenzi wake, yatakayomfariji na yatakayomfanya apende kuzungumza naye.

Mara nyingi mwanaume akiona mke au mpenziwe ni mtu wa kupenda chokochoko, mara nyingi humuepuka. Anajitahidi kadiri ya uwezo wake kukaa naye mbali. Ataona ni bora achelewe kurudi nyumbani akakutane na marafiki baa, wapige stori ili muda uende na akirudi nyumbani asiwe na muda wa kuzungumza na mwenzi wake, yeye ni kula na kulala.

2. KUTORIDHIKA

Wanaume wengi wanachukia kuwa na wanawake wasioridhika. Baadhi ya wanawake hata uwape nini huwa hawaridhiki. Wanawasumbua wapenzi wao kwamba hawawatimizii mahitaji. Mwanaume anajitoa kumpa zawadi mpenzi wake, haridhiki tu.

Anaanza kuikosoa. Anasema haifanani na yeye, eti si ya hadhi yake. Akipewa fedha anasema hazitoshi. Kila siku ni malalamiko. Hampi nafasi mpenzi wake ya kufurahia uhusiano wao.  Anamfanya kila anapokutana naye awaze atapigwa mzinga.

BONYEZA HAPA  UONE TABIA ZOTE

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.