Moshi. Jeshi la Polisi mkoani Kilimanjaro linawashikilia watumishi watatu wa Shule ya Sekondari Kisomachi, iliyopo Wilaya ya Moshi, Mkoani Kilimanjaro kwa uchunguzi wa tukio la vifo vya wanafunzi wawili wa kidato cha nne wa shule hiyo.
Watumishi hao wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani hapa ni mkuu wa shule hiyo, mwalimu wa zamu pamoja na mtunza stoo wa shule hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro (RPC), Simoni Maigwa imesema wanafunzi hao walifariki dunia Mei 12 shuleni hapo baada ya kuingia ndani ya tenki la kuhifadhia maharage baada ya sehemu ya chini ya kutolea maharage kuziba.
Wanafunzi waliofariki dunia ni Edson Gabriel Mosha (17) na Godwin John (17) ambao wote ni wanafunzi wa kidato cha nne katika shule hiyo.
“Wanafunzi hawa baada ya kuingia kwenye tenki kwa lengo la kutoa maharage kwenye tenki hilo baada ya sehemu ya chini inayotolea maharage kuziba, kwa hiyo baada ya kuingia ndani walikosa hewa na baada ya kutolewa walikimbizwa kituo cha afya Kirua Vunjo ambao ilibainika wameshafariki,” amesema.
Miili ya wanafunzi hao imehifadhiwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa ya Mawezi kwa uchunguzi zaidi.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







