Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Adolf Mkenda amesema Mitaala mipya ya Elimu ya Awali, Msingi, Sekondari na Ualimu itaanza kutumika baada ya Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023 kupitishwa na Mamlaka za maamuzi ambapo rasimu iliyopo inapendekeza Watoto waliopo darasa la tatu mwaka huu wasome mpaka darasa la sita kisha waende Sekondari, badala ya kuishia darasa la saba.
Prof. Mkenda amesema hayo Jijini Dodoma ambapo amesema tarehe rasmi ya kuanza kutumika kwa mitaala hiyo itatangazwa baada ya kupitishwa kwa Sera hiyo na kwamba itakapopitishwa utekelezaji utaanza kwa awamu.
Mkenda amesema rasimu hiyo inapendekeza Watoto waliopo darasa la tatu Mwaka huu 2023 ndio watakaosoma mpaka darasa la sita, hivyo wale waliopo darasa la nne, tano na sita wataendelea kusoma mpaka darasa la saba.
“Hatima ya yote utekelezaji huu unategemea Mamlaka ya Nchi itakaposema tuanze, matumaini yetu ni makubwa kwamba rasimu hii itapita na siku ya kutangazwa kuanza kwa utekelezaji itakuwa ni siku kubwa katika kuelekea mageuzi ya elimu nchini”
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







