Mama FeiToto
Taarifa za kuaminika kutoka chanzo cha karibu na familia ya kiungo wa kimataifa wa Tanzania, Feisal Salum “Feitoto”, zinaeleza kuwa mama mzazi wa mchezaji huyo amekataa kabisa kushiriki mazungumzo yoyote yanayohusiana na uhamisho wa mwanawe kurejea Yanga SC.
Inadaiwa kuwa Yanga imekuwa ikijaribu kwa njia mbalimbali kumshawishi Feitoto kurudi Jangwani, huku wakituma viongozi mbalimbali kwenda nyumbani kwao kumwomba msamaha kwa niaba ya wanachama na viongozi waliowahi kumkashifu hadharani.
Hata hivyo, mama mzazi wa Feitoto amekuwa mkali na amewafukuza baadhi ya wajumbe waliowasili kwa mazungumzo hayo, akisema hataki hata kusikia jina la Yanga.
Chanzo hicho kinasema msimamo huo umetokana na kile kilichoonekana kuwa ni dharau alizotendewa mwanae na baadhi ya wanachama na viongozi wa Yanga akiwemo msemaji wa klabu hiyo kipindi Feitoto alipoamua kuondoka Jangwani na kujiunga Azam FC.
Kwa sasa, taarifa za ndani kutoka kwenye kambi ya wawakilishi wa Feitoto zinaeleza kuwa nyota huyo ameshafikia makubaliano na klabu kubwa zaidi Afrika Mashariki kwa sasa Simba SC, ambayo pia inashikilia nafasi ya tano kwa ubora barani Afrika kulingana na viwango vya CAF.
Ujio wa Feitoto Simba unaonekana kuwa pigo kubwa kwa Yanga, ambao walikuwa na matumaini makubwa ya kumrudisha mchezaji huyo kwa msimu ujao. Mashabiki wengi wa soka wanatazamia kwa hamu kutangazwa rasmi kwa usajili huo unaoweza kuongeza moto mkubwa kwenye kikosi cha Simba SC
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






