Kipigo cha Simba chawaibua Zitto Kabwe, Naibu Waziri Mwana FA na Waziri Ummy Mwalimu

Admin Updates1 year ago4 Views

 Dar es Salaam. Saa chache baada ya mtanange wa Simba na Yanga kumalizika ambapo Yanga wameibuka na ushindi wa bao tano kwa moja, viongozi mbalimbali wameibuka na kutoa hisia zao kwenye mtandao wa X, (zamani Twitter).

Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameandika kwenye mtandao huo ujumbe unaosomeka, ‘Dunia ipasuke tuingie. Aibu hii naikabili vipi ee Mola’.
Zitto ameandika ujumbe huo saa 1:24 usiku, ambapo dakika chache baadaye Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu, alimjibu kwa kusema, ‘Kwa kweli leo tumeaibika’.
Mbali na Ummy, Naibu Waziri wa Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma maarufu kama Mwana FA, amenukuu ujumbe huo wa Zitto na kusema ‘5 nyingi sana kaka kusema la ukweli’.
Mchezo huo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu kubwa umemalizika huku Yanga ikipaa kileleni kwa kufikisha alama, 21 huku simba ikibaki na alama 18.
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.