Rapa wa Marekani, William Roberts II ‘Rick Ross’ ameeleza kuwa anajifua kuja kupanda Mlima Kilimanjaro, Januari mwakani, suala lililowaibua Watanzania mitandaoni kuhusiana na mlima huo.
Ross aliweka video mtandaoni akifanya mazoezi kujiandaa kupanda mpaka kileleni mwa mlima huo na kisha mtandao rasmi wa Rap kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ukaweka taarifa hiyo bila ya kueleza mlima huo unapatikana nchi gani.
Hilo lilifanya Watanzania ‘kuvamia’ ukurasa wa mtandao huo na kufafanua kuwa mlima huo upo Tanzania ikiwemo kuweka alama ya bendera ya Tanzania na wengine wakimkaribisha rapa huyo aliyewahi kushirikishwa na Diamond Platnumz kwenye Wimbo wa Waka waka uliotoka mwaka 2017.
Jack the Giant aliandika: “Mlima Kilimanjaro upo Tanzania, Mkoa wa Kilimanjaro, karibu Tanzania Rick Ross.” Naye Gerrard Smith alihoji: “Kusema (mlima) upo Tanzania hamuwezi sio?”
Mbali na hayo, maoni mengine yalikuwa ni ya kujivunia na kufurahia kwa Ross kuhitaji kupanda mlima huo wenye urefu wa meta 5,895 kutoka usawa wa bahari.
Aidha, mwaka jana Ross aliwahi kutoa ahadi ya kupanda mlima huo uliofunikwa na theluji alipokuwa akihojiwa na Full Send Podcast ikiwa pia ni miongoni mwa majaribio magumu anayopanga kuyafanya kila mwaka kwa ajili ya mashabiki wake.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







