Pichani ni Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor H. Seff na Mbunge wa Jimbo Mwanga Mhe. Joseph Tadayo walipotembelea ujenzi wa Makalavati Kumi na Sita (16) yanayojengwa kwenye Barabara ya Msuya yenye urefu wa kilometa 13.8 iliyopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro .
Akizungumza katika ziara hiyo ya Ukaguzi wa Miradi ilnayofanywa na Mtendaji Mkuu wa TARURA kujionea maendeleo ya utekelezaji wa Miradi ya TARURA Meneja wa TARURA Mkoa wa Kilimanjaro Mhandisi Nicholaus Francis amesema kwa Mradi huu unatekelezwa na muungano wa Wakandarasi wawili Wazawa (M/S Casco Construction na Bronze Tech Company Ltd) ambapo unaendelea vizuri ambapo Mtendaji Mkuu aliwataka Wakandarasi hao kumaliza kazi kwa Wakati kabla ya vipindi vya mvua kuanza mwezi Machi mwaka 2024.
Pichani pia katika
ziara yake mkoani Kilimnajaro Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini
na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor H. Seff wa kwanza kulia alifanya ukaguzi wa
mradi wa matengenezo ya barabara ya Kisangara kwenda Shighatini yenye urefu wa
Kilometa 25 inayotengenezwa na Kikundi Maalum cha kijamii (Special Group)
kiitwachoa Muhako Engineering (Labour base) katika Halmashauri ya Wilaya ya
Mwanga Mkoa wa Kilimanjaro tarehe 02.01.2024.
Mtendaji Mkuu alifurahishwa na
ushiriki wa Vikundi vya Kijamii katika utekalizaji wa Miradi ya Ujenzi na
Matengenezo ya Barabara. Mkurugenzi wa ufundi wa Kikundi cha Muhako Stephen
Mkeni alimueleza Mtendaji Mkuu wananchi katika eneo la mradi wameshirikishwa
vyema kwenye kazi zinazoendelea kwa kuwapatia ajira.
Hata hivyo, Mtendaji Mkuu
alilisitiza Halmashauri ya Mwanga kuhamasisha ushiriki wa vikundi vya Kijamii
kwenye kazi za ujenzi na Matengenezo ya Barabara ili kufika asilimia 30 ya
bajeti zinazotengwa kwa kazi za matengenezo ya barabara zitakazotekelezwa na
vikundi maalumu vya kijamii kila mwaka ili kuwawezesha kiuchumi na kuondokana
na umasikini.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33











