
Hakikisha unawakwepa aina hii ya wanawake ili usijiingize kwenye matatizo. Nitakwambia ni kwa nini…..1.Demu wako wa zamani
Ni
vizuri kutorudia mahusiano ya zamani na zaidi kama kwenye mahusiano
yenu ya mwanzo mambo hayakuishia kwa uzuri. Sababu kuu ya msingi,
kiukweli ni kwamba hakika mwanzoni mlikuwa hamuendani na ndio sababu ya
iliyopelekea kuvunjika kwa mahusiano yenu, ndani ya hizo sababu kuna
vitu vilivyopolekea kutokea kwa hayo, ukichunguza na kuziangalia kwa
makini utagundua ni za asili na ambazo si rahisi kwa mmoja wenu
kuzibadilisha sababu ni vitu au mambo ambayo yatakuwa ni ya damuni.
2.Dada wa rafiki yako kipenzi
Epukana
na kujiingiza kwenye mahusiano na dada wa rafiki yako. Si tu kwamba
utaweza kujiingiza kwenye uhasama na chuki kama mambo hayatakwenda sawa,
ila pia utaweza kujiweka kwenye mazingira ya kujikuta siku moja
unapigwa hata ngumi za uso sababu tu ulimuumiza dada yake. Pia, utaweza
kumkosa mtu ambaye ndie alikuwa ni kimbilio lako kwa mambo mbalimbali
pale ambapo itatokea wewe na dada yake mambo kutokwenda sawa, sababu
hapo patakuwa na mgongano wa kimaslahi kwa huyo rafiki yako.
3.Wanawake wenye mambo mengi
Kiukweli,
kutoka na watu kama hawa kinaweza kuwa ni kitu cha kufurahisha, ila
mwisho wa siku itakuingiza kwenye matatizo. Mara zote kumbuka ni vyema
kuwa salama kuliko kujuta. Usijiingize kwenye majaribu ambayo utakuja
kuyajutia kwa maisha yako yote.
4.Wanawake wanaopenda hela kupitiliza (Wachunaji)
Kuwa
mbali nao, labda kama unataka salio lako limalizike pasipo wewe
kujifahamu. Naamini hili kila mmoja analifahamu na halihitaji darasa
zaidi.
5.Demu wa zamani wa rafiki yako
Kama unathamini
urafiki wako na mshikaji wako achana na habari ya kutoka na aliyekuwa
demu wake. Mambo yanaweza kubadilika na kuwa kama au zaidi ya
yaliyotokea kwa rafiki yako na ikaja kula kwako zaidi. Wakati mwengine
inaweza tengeneza chuki kati yako na rafiki yako, huku akiamini kwamba
ulikuwa unatoka au kumnyemelea demu wake toka zamani.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






