Mhandisi Victor Seff akagua Barabara Kijiji cha Msomera Handeni Mkoani Tanga,Alipongeza JWTZ

Admin Updates1 year ago7 Views

 

Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za
Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor H. Seff ametembelea miundombinu ya
barabara za Kijiji cha Msomera ambapo ni moja ya eneo maalumu lililotengwa na
Serikali kwa ajili ya kuwahamishia wafugaji waliokuwa wakiishi katika hifadhi
ya Ngorongoro.
 

Msimamizi wa Ujenzi wa Mradi wa Makazi ya
Wafugaji Kanali S.E Mihayo amempongeza Mhandisi Seff kwa ushirikiano mkubwa
unaotolewa na watendaji wa TARURA na akimpongeza Meneja wa Wilaya ya Handeni
Mhandisi Eng. Judica Makyao kwa kujitoa kikamilifu kuhakikisha barabara
zinafunguliwa na kupitika katika eneo la mradi.

Kanali Mihayo alimueleza Mhandisi Seff eneo
la Mradi linahusisha Halmashauri tatu (3) za Wilaya za Handeni, Kilindi na
Simanjiro. Alieleza kuwa, utekelezaji rasmi wa ujenzi wa nyumba za Makazi
umeanzia katika eneo la Msomera, Wilaya ya Handeni na kwa sasa takribani
barabara zote muhimu zimefunguliwa na TARURA. 
Kanali Mihayo alimuambia Mhandisi Seff kuwa, awamu ya pili ya ujenzi wa
nyumba utafanyika katika Wilaya ya Kilindi na Simanjirio. Kanali Mihayo
alieleza kuwa kwa sasa wataamu wa kupanga matumizi ya ardhi “Surveyor”
wanaendelea na zoezi la kuzitambua barabara katika eneo la Kilindi na Simanjiro
ili ziweze kufunguliwa na kuendelea na ujenzi.

 Meneja wa TARURA wa Wilaya ya Hendeni
Mhandisi Judica Makyao alimuambia Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff
kuwa, mtandao wa barabara katika Kijiji cha Msomera unajumla ya kilometa 986,
ambapo jumla ya kilometa 186 za barabara zimekamilika kuchongwa na kilometa 24
zimewekewa kifusi na changarawe. Alieza kuwa Mkandarasi yupo eneo la kazi na
kuendelea na ufunguzi wa barabara pamoja na ujenzi wa Makalavati 10 katika
Kijiji cha Msomera

Mhandisi Seff alimpongeza Kanali Mihayo kwa
kazi kubwa wanayoifanya ya Ujenzi wa Makazi ya Wafugaji na kumuahidi TARURA
itaendelea kutoa ushirikiano mkubwa na kuhakikisha ujenzi wa barabara unakuwa
wa viwango vilivyokusudiwa ili  kufikia
adhima ya malengo mazuri ya Serikali inayoongozwa na Mhe.  Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania.

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...