LOWASSA AWATAKA WATANZANIA KUCHANGAMKIA FURSA ZA AJIRA ZITOLEWAZO NA AFRIKA MASHARIKI

Admin Updates9 years ago6 Views

Sehemu ya wananchi wa eneo la Kisongo, Jijini Arusha wakiwa wamefunga barabara kuzuia msafara wa Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, ili waweze kumsalimia na kumsikiliza, wakati alipokuwa njiani kuelekea eneo la Ngaramtoni mpaka Namanga, kwenye Mkutano wa Kampeni, leo Oktoba 7, 2015.PICHA ZOTE NA OTHMAN MICHUZI, ARUSHA.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa kwa vijana wa eneo la Kisongo, walipokuwa wakimsindikiza mpendwa wao.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwasili kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Mringa, Jimbo la Arumeru Magharibi, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake. 
WATANZANIA wametakiwa kujifunza kuchangamkia fursa za ajira zinazotolewa na Afrika Mashariki kama ilivyo kwa nchi nyingine.

Kauli hiyo ilitolewa jana na mgombea wa Urais kupitia Chadema, Edward Lowassa alipokuwa kwenye kampeni zake zilizofanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Namanga.

Lowassa alisema iwapo atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atahakikisha kuwa watanzania wanachangamkia fursa za Afrika Mashariki kama ilivyo kwa Kenya.

“Napenda mahusiano ya Afrika Mashariki yawe ya kweli na siyo upande mmoja unafaidi na mwingine haufaidi,”alisema na kuongeza kuwa:

“Watanzania wakiwa wanapita kwenye mpaka wa Namanga wasisumbuliwe wapite bila shida.”
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Jimbo la Arumeru Magharibi waliohudhulia Mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Mringa, Jimbo la Arumeru Magharibi, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwahutubia wananchi wa Jimbo la Arumeru Magharibi katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Mringa, Jimbo la Arumeru Magharibi, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwapungia wananchi wa Jimbo la Longido waliohudhulia Mkutano wa Kampeni zake, uliofanyika kwenye Uwanja wa Namanga, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015.
Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, akiwasalimia watoto walikuwepo kwenye Mkutano huo.
Lowasaaaaa……   Mabadilikoooooooo……
Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akiwasalimia wananchi wa Mji wa Namanga, katika Jimbo la Longido, wakati wa Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kupitia mwamvuli wa UKAWA, Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Namanga, Jijini Arusha leo Oktoba 7, 2015.
Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.