Mchungaji ‘TB Joshua’ akisalimiana na rais Kikwete.
HATIMAYE, Mwangalizi Mkuu wa Kanisa la Scoan (Synagogue Church of All Nations), Mtume na Nabii Temitope Balogun Joshua ‘TB Joshua’ ametua Bongo juzi akitokea nchini Nigeria, maalum kumshuhudia Rais Mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli ‘JPM’ akiapishwa leo.TB Joshua aliwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kupokelewa na JPM akiwa ameongozana na mkewe, mama Janeth Magufuli na wasaidizi wengine wa JPM.
Kwa mujibu wa Wabongo waliobahatika kusalimiana na TB Joshua kwa kushikana mikono, ujio wa nabii huyo umeonesha alivyoshindwa kulala nchini mwake wakati Magufuli akiapishwa jijini Dar, ikizingatiwa kuwa, alimtabiria kushinda nafasi hiyo ya urais.
“Jamani, naye (TB Joshua) kajisikia raha Magufuli kushinda. Mtu aliyemtaribiria kuwa rais, kashindwa kulala nchini mwake, akaona aje aone kama ni kweli,” alisema mfanyakazi mmoja wa uwanja huo wa ndege.
Mara baada ya kutua uwanjani hapo, TB Joshua alikwenda Ikulu ya Magogoni, Dar kwa ajili ya kumsalimia rais anayemaliza muda wake leo, Dk. Jakaya Kikwete ‘JK’, pia kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa uhuru na amani.
Katika neno lake la moyoni kama nabii, TB Joshua alisema Dk. Magufuli ndiye rais mwenye neema, baraka na fanaka kwa Watanzania.Wakati huohuo, leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar, Dk. Magufuli anaapishwa kuwa Rais wa Tanzania na hivyo kuanza kuandika siku yake ya kwanza kuwa ikulu.
Kwa mujibu wa itifaki, mteule huyo na aliyekuwa mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassan wataingia uwanjani hapo kabla ya JK, lakini mara baada ya kuapishwa, Dk. Magufuli atakuwa wa kwanza kutoka akiwa katika msafara wenye ulinzi mkali kuelekea ikulu kwa maisha rasmi ya urais.
Aidha, Dk. Magufuli atafuatiwa na makamu wake kabla ya viongozi wengine wakiwemo marais wastaafu.
Tukio kama hilo liliwahi kufanyika mwaka 2005 wakati JK alipoapishwa kuchukua nafasi ya rais aliyemaliza muda wake, Benjamin William Mkapa.
Kwa mujibu wa Wabongo waliobahatika kusalimiana na TB Joshua kwa kushikana mikono, ujio wa nabii huyo umeonesha alivyoshindwa kulala nchini mwake wakati Magufuli akiapishwa jijini Dar, ikizingatiwa kuwa, alimtabiria kushinda nafasi hiyo ya urais.
“Jamani, naye (TB Joshua) kajisikia raha Magufuli kushinda. Mtu aliyemtaribiria kuwa rais, kashindwa kulala nchini mwake, akaona aje aone kama ni kweli,” alisema mfanyakazi mmoja wa uwanja huo wa ndege.
Mara baada ya kutua uwanjani hapo, TB Joshua alikwenda Ikulu ya Magogoni, Dar kwa ajili ya kumsalimia rais anayemaliza muda wake leo, Dk. Jakaya Kikwete ‘JK’, pia kumpongeza kwa kufanikisha uchaguzi mkuu kwa uhuru na amani.
Katika neno lake la moyoni kama nabii, TB Joshua alisema Dk. Magufuli ndiye rais mwenye neema, baraka na fanaka kwa Watanzania.Wakati huohuo, leo kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar, Dk. Magufuli anaapishwa kuwa Rais wa Tanzania na hivyo kuanza kuandika siku yake ya kwanza kuwa ikulu.Kwa mujibu wa itifaki, mteule huyo na aliyekuwa mgombea mwenza, Samia Suluhu Hassan wataingia uwanjani hapo kabla ya JK, lakini mara baada ya kuapishwa, Dk. Magufuli atakuwa wa kwanza kutoka akiwa katika msafara wenye ulinzi mkali kuelekea ikulu kwa maisha rasmi ya urais.
Aidha, Dk. Magufuli atafuatiwa na makamu wake kabla ya viongozi wengine wakiwemo marais wastaafu.
Tukio kama hilo liliwahi kufanyika mwaka 2005 wakati JK alipoapishwa kuchukua nafasi ya rais aliyemaliza muda wake, Benjamin William Mkapa.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33