Baada ya lile drama kati ya star wa Bongo movie, Niva Supermariyo, na Nay wa Mitego kushika moto kutokana na wimbo wa ‘Shika adabu yako’ ya Nay na Niva kuamua kumjibu kupitia filamu ambayo aliipa jina la ‘Maisha ya mtoto wa Manzese’
Sasa mastaa hao wameamua ‘kuvuana nguo’ hadharani kwa kila mmoja kuamua kumponda mwenzake.
Wakizungumza na Enewz kwa wakati tofauti tofauti ili mastar hao waweke bayana tofauti zao lakini waliamua kutoleana uvivu kwa kupigana madongo ya live bila kukwepeshana.
Alipoulizwa Niva kwanini aliamua kuingia kambi ili kuandaa filamu tu itakayo mponda Nay? Niva alisema “Nay ni kama babaji kwahiyo hawezi shindana na mimi haniwezi kama yeye alizoea kuwaonea wanyonge mimi sasa haniwezi ,kimaisha kwanza hajanifikia na mtu mwenye akili huwezi kujianika sana vitu vyako vya ndani kama yeye anajiona star, kwanini anakimbiwa na wanawake”.
Enewz haikuishia kufanya mahojiano na Niva, Ilimlazimu kumtafuta Rapper Nay Wamitego kujua nini mtazamo wake kuhusu maneno ya Niva. Nay Wamitego alifunguka maisha anayo ishi Niva pamoja na gari alilopewa na Muhindi.
“Kwa sehemu ambayo ninau hakika nayo kwa asilimia mia moja ni kwa Niva, Niva hana geto ana gari na alipewaga na Muhindi, alipeleka movies namfahamu vizuri, Mimi natokea mtaani naimba sifanyi movie kwahiyo siishi maisha ya kuigiza”. Alisema Nay.
Aidha Niva ametoa sababu ya kutokuwepo sokoni kwa movie hiyo hadi sasa ni kutokana na kuzuiwa na uongozi wake baada ya kuona haina maana kutengeneza filamu kwa lengo la kujibishana na mtu na kumwambia kuwa anayeanza anaweza asionekane mgomvi ila anaye malizia akaonekana kuwa ndio mgomvi. Lakini amesema kuwa Nay wa mitego akiendelea ataiachia tuu huku Nay akimtaka Niva kuonyesha mahali anapoishi kama alichoimbwa ni uongo.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33






