MAHUSIANO:Unaambiwa mwanawake Kama Unampenda Mumeo, Mpende na Mama Mkwe..Soma zaidi hapa

Special Correspondent6 years ago7 Views

Habari wakuu,

Kumekua na tabia kwa baadhi ya wanawake ya kupenda waume zao na kuwachukia wazazi wa kike wa wawaume zao.


Hii tabia imekithiri katika baadhi ya ndoa nyingi, wanawake hao wamekua wabinafsi sana, hawataki kuendeleza mahusiano ya mume wake na familia ya mumewe.


Mfano, unakuta mtoto huyo wa kiume ni tegemeo la nyumbani kwao au wakati mwingine sio tegemeo ila lazima atume kiasi flani cha matumizi nyumbani kwao, lakini mkewe akiona hivyo anazuia hataki pesa zitumwe kwa mama mkwe.


Wakati mwingine mama huyo anaumwa na anahitaji kuja kutibiwa kwa mwanae, lakini mwanamke anakasirika na kumwambia mumewe asije kupata matibabu nyumbani kwao.


Wanawake wengine wamekua wakigombana na mama wa waume zao bila hata aibu, lakini eti akiwa na mumewe anampenda. Wanawake wenzangu tujifunze kuwaheshimu mama wa waume zetu na tuwapende kama mama zetu.


Kama unampenda mumeo, mpende na mama mkwe


Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K

Stay Informed With the Latest & Most Important News

I consent to receive newsletter via email. For further information, please review our Privacy Policy

Categories
Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.