Sheria mpya nchini Saudia inawalinda wanawake kutopewa talaka bila kujua. Kuanzia siku ya Jumapili , mahakama zitatakiwa kuwaelezea wanawake kupitia njia ya ujumbe wa simu kwamba wamepewa talaka.
Mawakili wanawake wanapendekeza kuwa hatua hiyo itamaliza kile kinachotajwa kuwa talaka za siri ambapo wanaume hutoa talaka bila kuwaelezea wake zao.
Amri hiyo itahakikisha kuwa wanawake wanajua hali ya ndoa yao na itawalinda dhidi ya masurufu,
Mwaka uliopita marufuku ya wanawake kuendesha magari iliondolewa na mahakama nchini Saudia.
Hatahivyo wanawake bado wako chini ya usimamizi wa wanaume.
”Sheria hiyo mpya itahakikisha kuwa wanawake wanapewa haki zao za masurufu wakati wanapopewa talaka”, alisema wakili Nisreen al-Ghamdi.
Pia ina hakikisha kuwa uwezo wowote utakaotolewa na mahakama hautumiki vibaya.
”Wanawake wengi wamewasilisha malalamisihi yao katika mahakama za rufaa kwa kupewa talaka bila ya wao kujua” , kulingana na wakili Samia al-Hindi.
Hatua hiyo mpya inasemaekana kuwa miongoni mwa mabadilikio ya kiuchumi na kijamii yalioshinikizwa na mwanamfalme Mohammed bin Salman, ikiwemo kuwaruhusu wanawake kuingia uwanjani na kutazama mechi za kandanada mbali na kufanya kazi ambazo awali zimekuwa zikifanywa na wanaume pekee.
Ni mambo gani ambayo wanawake wa Saudia hawawezi kufanya?
Kuna vitu vingi ambavyo wanawake wa Saudia bado hawaruhusiwi kufanya bila ya kuomba ruhusa kutoka kwa wasimamizi wao wa kiume kama vile waume zao , baba zao ndugu wa kiume ama watoto wao.
Vitu hivyo ni:
Kuwasilisha maombi ya pasipoti.
Kusafiri katika mataifa ye kigeni.
Kuolewa
Kufungua akaunti ya benki.
Kuanzisha biashara
Kuondoka jela
Hali hiyo ya kusimamiwa na wanaume imesababisha taifa hilo kuwa miongoni mwa mataifa ambayo usawa wa kijinsia umekandamizwa mashariki ya kati.
from UDAKU SPECIAL BLOG http://bit.ly/2CU3P4x
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33





