Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mwanadada, Paskazia Andrew Sindano (17) kwa tuhuma za mauaji ya mtoto Kashindye Mgemagiko (03) kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi.
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Simon
Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga, Simon Haule
Taarifa iliyotolewa Jana Februari 17, 2019 na kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga, Simon Haule imeeleza kuwa tukio hilo lilitokea juzi Ijumaa saa 12 jioni katika kitongoji cha Emalaupena kijiji cha Misayu kata ya Ubagwe, halmashauri ya wilaya ya Ushetu.
“Chanzo cha tukio hili ni wivu wa kimapenzi kwa kuwa mama wa mtoto aliyeuawa inasemekana alikuwa na mahusiano ya kimapenzi na mume wa Paskazia na kupelekea kuzaliwa mtoto huyo,” amesema Kamanda Haule.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa mbinu iliyotumika ni ya kumkata panga kichwani nje ya nyumba yake.
Kamanda Haule amesema kuwa kwa sasa mwili umehifadhiwa na mtuhumiwa atafikishwa mahakamani mara moja.
Kwa upande mwingine, Kamanda Haule amewataka wananchi kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake wapeleke malalamiko, kero na migogoro yao katika ofisi za serikali ya kijiji au mabaraza ya wazee ili kuepuka vitendo vya kikatili.
from UDAKU SPECIAL BLOG https://www.udakuspecially.com/2019/02/amuua-kwa-panga-mtoto-wa-jirani-kisa.html
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







