Mfahamu Mtanzania Aliyeigiza wenye Game of Throne

7 years ago92 Views

Imezoeleka kuona watu wa kutoka mataifa mengine wakifanya vizuri kwenye tasnia ya filamu duniani kupitia kiwanda cha filamu nchini Marekani Hollywood, lakini ni mara chache sana kuona watu kutoka Afrika wakifanya vizuri.

Hii imekuwa tofauti sasa, kwani hata Tanzania ambayo imezoelekea kukaa nyuma kwenye tasnia ya burudani dunaini, imefanikiwa kupenyeza mtu na kuipeperusha vyema bendera ya nchi, japokuwa sio moja kwa moja.

Anaitwa Lucian Gabriel Wiina Msamati, aliyezaliwa Machi 5 1976 huko Uingereza, na wazazi wake ni Watanzania kabisa, baba na mama yake, ambao walikuwa na wahudumu wa afya, akiwa mtoto wa kwanza kati ya watoto wanne.  Elimu yake ya msingi aliipata hapo Olympio jijini Dar es salaam, na kisha wakahamia Harare Zimbabwe, na kusoma katika shule ya Avondale, kisha kuendelea na elimu yake ya juu huko huko Zimbabwe.

Baada ya hapo Msamati alianza kazi kwenye ‘media’ kama mwandishi wa habari wa kujitegemea na kwenye kampuni mbali mbali za matangazo, huku akijihusisha na sanaa za majukwaani (theatrical).

Alipoanza kupata mafanikio kwenye sanaa ya filamu, Msamati alipata deals mbali mbali za kuigiza kwenye filamu kubwa kama Doctor Who, Luther, na Game of Throne ambayo bado inaendelea kutengenezwa muendelezo wake.

Kwa sasa Msamati amehamia nchini Uingereza na anaishi huko, tangu alipofanya uamuzi huo mwaka 2003, na kufanya kuwa mmoja wa waigizaji wakubwa wenye asili ya Tanzania, ambao nchi inapaswa kujivunia.

 Manchester United yakabiliwa na deni kubwa | East Africa Television
Kuelekea mchezo wa kombe kongwe zaidi nchini England na pengine duniani kwa ujumla (FA Cup), kati ya wenyeji Chelsea dhidi ya Manchester United, Man United wanakabiliwa na deni la kulipa mbele ya Chelsea.

from UDAKU SPECIAL BLOG http://bit.ly/2V0apN8
via

0 Votes: 0 Upvotes, 0 Downvotes (0 Points)

Join Us
  • Facebook38.5K
  • X Network32.1K
  • linkedin12.6k
  • youtube23.4k
  • Instagram18.9K
Mchanganyiko

Loading Next Post...
Follow
Sign In/Sign Up Search Trending 0 Cart
Popular Now
Loading

Signing-in 3 seconds...

Signing-up 3 seconds...

Cart
Cart updating

ShopYour cart is currently is empty. You could visit our shop and start shopping.