
Mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu
Mbunge wa Singida Mashariki na Mnadhimu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Tundu Lissu amejitokeza na kumtakia heri Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa kufuatia uamuzi wake wa kurejea Chama Cha Mapinduzi.
Lowassa ametangaza kurejea CCM mapema Machi 1, 2019 ambapo alipokelewa na Mwenyekiti wa Chama hicho Dkt, John Pombe Magufuli katika ofisi ndogo za makao makuu ya chama hicho yaliyopo Lumumba Jijini Dar es salaam.
Lissu ameandika, “Edward Lowassa mwenyewe amesema amerudi nyumbani, maana yake ni kwamba alikuwa ‘ugenini’ tangu Julai 2015. hakuwahi kutuhonga wala kununua chama chetu kama tulivyotukanwa huko nyuma”.
“Tulimkaribisha na kumpatia majukumu ya kutuongoza kwenye mapambano ya 2015. na alitekeleza majukumu hayo vizuri kwa kadri alivyoweza, na kadri tulivyomwezesha. matunda ya kazi yake, na ya kazi yetu yanajulikana”, ameandika Lissu.
Lissu ameongeza kuwa, “na pengine sasa wataacha kumtishia kumnyang’anya mafao yake ya kisheria kama Waziri Mkuu mstaafu, badala ya kumlaani kwa kuondoka kwetu ‘ugenini’, mimi namtakia kila la kheri na mapumziko mema ‘nyumbani’ kwake sisi tutaendelea na safari yetu ya Canaan”.
Wakati akipokelewa na uongozi mkuu wa CCM, Lowassa mwenyewe hakubainisha nini sababu ya kurejea CCM, bali aliishia kusema kuwa amerudi nyumbani.
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/2ELWtkv
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33





