
Siku chache baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli kuibua maswali juu ya tukio la kutekwa Mfanyabiashara Mohamed Dewji Kamanda wa Polisi Dar es salaam Lazaro Mambosasa amejitokeza na kusema yeye alishamaliza kazi yake.
Mambosasa amesema baada ya yeye kumaliza kazi yake alikabidhi kwa viongozi wake wa juu na kwa sasa wanaojua kinachoendelea ni Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ambaye anatakiwa kutoa taarifa za uchunguzi zilizowasilishwa kwake.
Mambosasa amesema, “kuhusu maelekezo ya Rais aliyoyatoa kuhusu kutekwa kwa Mo, maadamu aliyatoa mbele ya Mkuu wetu wa Jeshi la Polisi na DCI ambao walikuwepo, jalada hilo lilishafika kwao, huko ndiko wanakojua kinachoendelea”.
“Mimi jukumu langu lilishakwisha kwa hiyo ni suala la maamuzi ya juu kuhusu hatua zilizofikiwa kwenye jalada hilo”, ameongeza Kamanda Mambosasa.
Mapema juzi Ikulu akiwaapisha Makamshna wa juu wa Jeshi la Polisi, Rais Magufuli alisema, “Jeshi la Polisi linatakiwa kuelewa kuwa Watanzania sio wajinga, kama suala la kutekwa kwa Mo Dewji linaacha maswali, tuliambiwa alitekwa na wazungu lakini lilipoisha haikueleweka, mwishoni aliyetekwa alionekana anakunywa chai na Mambosasa.”
from MALUNDE 1 BLOG https://ift.tt/2H5pUjK
via
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33





