Berega, Kilosa 02.08.2024
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amempongeza Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) Mhandisi Victor H. Seff kwa kazi nzuri TARURA wanayofanya Tanzania nzima.
Rais Samia ameyasema hayo Jana wakati akiongea na wananchi wa Berega wilayani Kilosa mara baada ya kufungua daraja la Berega lililojengwa na TARURA.
Rais Samia alisema anaipongeza TAMISEMI kwa kazi wanayoendelea kufanya ikiwemo uendelezaji wa miundombinu maeneo ya vijijini kupitia TARURA.
“Nimpongeze sana sana Mhandisi Seff, wataalam na timu yake ndani ya TARURA kwa kazi nzuri wanayoifanya Tanzania nzima, nimemvisha maua yake”.
Aidha, ameishukuru kampuni ya kizalendo ya Nyanza Road Works Limited na kampuni ya kizalendo ya SMARCON kwa kushirikiana na Pendharkar & Associates Limited kwa usimamizi wa mradi huo.
“Nawashukuru wakandarasi na wasimamizi wote kwa ujenzi wa daraja hili zuri”, amesema Rais Dkt. Samia.
Amesema kwamba daraja hilo litasaidia kuwaunganisha wananchi lakini kurahisisha upatikanaji wa huduma za kijamii.
Hata hivyo amewataka wananchi kutunza daraja hilo na amewaomba wasichimbe michango ili liweze kutumika miaka mingi kwa vizazi na vizazi.
Pia amewataka wananchi kutoharibu mazingira ya mto huo na wasichimbe mchanga chini ya daraja hilo kwani kwa kufanya hivyo watalipunguzia nguvu daraja hilo na pia kutanua mto.
“Wananchi mnaharibu mazingira, fanyeni shughuli zenu kwenye mto lakini msiharibu mazingira msichimbe mchanga kwenye mto huu, daraja hili limechukua fedha nyingi ili wananchi mnufaike, tunzeni daraja hili “, alisisitiza
Ameongeza kusema kwamba wananchi watakapochimba mchanga ndani ya mto watapunguzia nguvu daraja hilo.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33







