Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini Mhandisi Victor H. Seff ametekeleza ahadi ya kuhakikisha Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) kupitia mradi wa RISE imetoa mafunzo maalum kuhusu masuala ya unyanyasaji wa kijinsia na usawa wa jinsia katika utekelezaji wa mradi wa RISE.
Mhandisi Seff kwa kushirikiana na Taasisi za kitaalamu zinazotoa elimu kuhusu kuhakikisha ukatili wa kijinsia unakomeshwa hasa maeneo ya kazi amesema TARURA kama mdau wa maendeleo ya Nchi ni Rai na lengo lao kuona vitendo vya ukatili wa kijinsia havina nafasi kwa jamii kwani TARURA inathamini mchango wa kila mmoja katika kuhakikisha ukatili wa Kijinsia unakomeshwa.
Akitoa mada juu ya namna ya kushughulikia masuala hayo nyeti ya ukatili wa kijinsia, Mtoa Mada Bi. Beatrice Mchome amesisitiza katika kushughulikia malalamiko yote yanayopatikana kutoka kwa wananchi kwa usiri na utu wa hali ya juu.
Pamoja na mambo mengine mafunzo hayo yamelenga pia katika kuwajengea uwezo watumishi hao kwa namna bora ya kushughulika na malalamiko hata yanayotokea kati ya mtumishi moja na mwingine kwani kutoshughulikia kunaweza sababisha kupunguza ufanisi wa watumishi hao kwenye mradi.
Naye, Mratibu wa Mradi wa RISE unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, Mhandisi Joel Lwitiko Mwandobo (pichani) kwa niaba ya watumishi amemshukuru Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor Seff kwa kuwawezesha wawezeshaji na kuhakikisha watumishi wanapatiwa mafunzo hayo muhimu ambapo amesisitiza kwa watumishi hao kufanya kazi kwa bidii na kila mtumishi kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Mafunzo hayo ya siku mbili yamefanyika katika Hoteli ya Midland jijini Dodoma na kuhudhuriwa na wataalam i mbalimbali ambao ni watumishi wa TARURA.
Recommended Products
-
2025 Summer Rapper Feid Ferxxo Men’s Cotton Fashion Hip-hop T-shirt Casual and Comfortable Short-sleeved T-shirt Street Wear
Affliate products $22.00 -
3 IN 1 Magnetic Folding Wireless Charger Station For IPhone Transparent Fast Charging For IWatch And Airpods
Affliate products -
Grandpa Of Love hoodies Human French Letters Dad Papa Papy Gift Men Clothing hoodies
Affliate products $22.00 -
Sale!
Lenovo D18 Drone 8K Aerial HD Dual-Camera Intelligent Obstacle Avoidance Brushless Power 5G WIFI Screen Remote Control GPS Drone
Affliate products Original price was: $7.99.$7.89Current price is: $7.89. -
Mini Portable Face Cordless Shavers Rechargeable USB Electric Shaver Wet & Dry Painless Small Size Machine Shaving For Men
Affliate products $44.00 -
New Original T75 Bone Conduction Wireless Bluetooth 5.3 Headphones Sports Earphones HiFi Sound Quality Waterproof TWS Headset
Affliate products $3.33








